UNHCR yataka msaada zaidi kwa warundi wanaorejea nyumbani Burundi
Akihiiitmisha ziara ya siku mbili nchini Burundi, Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Filippo Grandi, amepongeza juhudi zilizofanywa kusaidia wakimbizi kupata suluhu ya muda mrefu katika taifa hilo ambalo ni kiini cha ukanda wa Maziwa Makuu.