Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

22 MEI 2024

22 MEI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia huduma za afya kwa watoto nchini Haiti na simulizi afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO kuhusu yanayoenndelea Gaza. Makala tnakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni? 

  1. Ghasia zikiwa zinaongezeka katika mji mkuu wa Haiti, Port-Au-Prince, hospitali sita kati ya kumi nchini humo ziko katika hali mbaya ya utoaji huduma limeonya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF. 
  2. Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO aliyerejea hivi karibuni kutoka Ukanda wa Gaza amesimulia yale aliyoshuhudia akiwa huko huku huku akisisitiza kuwa "hakuna mahali salama" katika Ukanda huo na aliyoshuhudia ni “yakusitikisha na ya kutisha.”
  3. Makala inatupeleka Kaunti ya Garisa nchini Kenya ambako waathirika wa mafuriko na maporomoko ya udongo ya hivi karibuni walio katika makambi za muda za wakimbizi wa ndani wanapokea msaada wa fecha na vocha kutoka kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wake ikiwaweze kujikimu.
  4. Na mashinani tutaelekea nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
10'29"