Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

01 APRILI 2024

01 APRILI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu Gaza, na jitihada za kukabili habari potofu nchini DR Congo. Makala tunaku[eleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?

  1. Mratibu Mkuu wa Misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths amesema shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA ni uti wa mgongo wa operesheni za Kibinadamu Gaza hivyo jaribio la kulitenga shirika hilo lazima likome.
  2. Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kituo kilichojengwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO kimesaidia vijana kukabiliana na habari potofu na za uongo ambazo huchochea ukosefu wa amani kwenye taifa hilo la Maziwa Makuu barani Afrika. 
  3. Katika makala Assumpta Massoi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Kenya, anakupeleka kaunti ya Wajir kuona jinsi mradi wa maji ulivyoleta matumaini kwa familia na jamii.
  4. Na mashinani tutaelekea nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu afya kwa watoto.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
11'10"