Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

26 MACHI 2024

26 MACHI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DR Congo ambako Umoja wa Mataifa unasema wananchi milioni 23.4 wanakabiliwa na njaa. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu SEA, machafuko DRC na vifo vya wahamiaji. Mashinani inamulika miradi ya maji nchini Tanzania. 

  1. Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Hatua Maalum za Ulinzi dhidi ya Unyonyaji na Unyanyasaji wa Kingono imewekwa wazi hii leo.
  2. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) limetoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka kutokana na ongezeko la hatari kwa watu waliokimbia makazi yao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. 
  3. Na wakati mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) unaohusu Wahamiaji Wasiofahamika waliko ukitimiza miaka kumi, ripoti mpya ya shirika hilo iliyopewa jina ‘Muongo mmoja wa kukusanya taarifa za vifo vya wahamiaji’ inaonesha mienendo ya kutisha ya vifo na kupotea kwa wahamiaji katika muongo mmoja uliopita na kwamba mtu mmoja kati ya watatu hufariki duniani katika harakati za kukimbia migogoro katika nchi yake.
  4. Katika mashinani tunakuletea ujumbe wa Mhandisi Denis Arbogast, Msimamizi wa mradi wa maji Kasulu mkoani Kigoma nchini Tanzania, mradi inayofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wake.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
10'35"