Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

vifo

Mafuriko yamekumba maeneo ya kaskazini mashariki mwa Libya.
© National Meteorological Centre, Libya

Takriban watu 3, 000 wamekufa na 10,000 hawajulikani waliko kufuatia mafuriko Libya:WMO/WHO/IOM/IFRC

Mafuriko makubwa yaliyoikumba Libya tarehe 10 September yamesababisha maafa ikiwemo vifo vya takriban watu 3,000 na wengine zaidi ya 10,000 kutojulikana waliko Mashariki mwa nchi hiyo  kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu IFRC na mwezi mwekundu.

19 Novemba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo leo Flora Nducha anakuletea mada kwa kina ikijikita kuangalia changamoto zinazowakabili wakimbizi wa ndani ikiwemo huduma ya vyoo eneo la Uvira nchini DRC wakati dunia leo ikiadhimisha siku ya choo.

Sauti
10'50"
Huduma za dharura baada ya ajali kutokea katika moja ya maeneo ya mji wa New  York, nchini Marekani. Huduma za haraka huokoa maisha lakini pia UN inataka hatua madhubuti kuzuia ajali hizo.
UN News/Vibhu Mishra

Kila sekunde 24 mtu 1 hupoteza maisha katika ajali barabarani:Guterres 

Hatua za haraka zinahitajika na kusalia kuwa za muhimu sana katika kuokoa maisha ya maelfu na maelfu ya watu yanayopotea kila siku katika ajali za barabarani. Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe maalum wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya usalama barabarani ambayo kila mwaka huadhimishwa Novemba 17. “Natoa wito kwa kila mtu kujiunga nasi katika kushughulikia changamoto ya kimataifa ya janga la usalama barabarani.”