Wakati zahma zikiongezeka Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara na kuwalazimisha mamilioni ya watu kufungasha virago, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetoa raia ya kuongeza juhudi za kuwasaidia wakimbizi na wahamiaji hasa wanaobidi kupitia njia hatari kwenye bahari ya Mediterrania kwenda kusaka mustakbali bora.
Kufuatia ajali nyingine ya boti iliyokatili maisha ya watu 43 siku ya Jumatatu kwenye pwani ya Libya, mashirika ya Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM na lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR yametoa wito kwa nchi kurejea operesheni za kuwasaka na kuwaokoa watu kwenye bahari hiyo.
Kutana na muhamiaji Mohamed Ahmed Bushara aliyekwenda kusaka maisha Libya miaka mitano iliyopita lakini hali ngumu, ubaguzi , machafuko na kuwekwa rumande vilimkatisha tamaa ya kukimbiza ndoto hiyo na akakata shauri kurejea nyumbani Sudan kushika ustaaranu mwingine kwa msaada wa shirika la Umoja
Kutana na muhamiaji Mohamed Ahmed Bushara aliyekwenda kusaka maisha Libya miaka mitano iliyopita lakini hali ngumu, ubaguzi , machafuko na kuwekwa rumande vilimkatisha tamaa ya kukimbiza ndoto hiyo na akakata shauri kurejea nyumbani Sudan kushika ustaaranu mwingine kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM na Muungano wa Ulaya.
Ujira wa wahamiaji ugenini kwa wastani ni chini ya asilimia 13 kulinganisha na wafanyakazi wenyeji katika nchi za kipato cha juu, imesema ripoti mpya ya shirika la kazi la Umoja wa Mataifa, ILO, iliyotolewa leo mjini Geneva, Uswisi.
Mtoto mhamiaji kutoka nchini Ghana ambaye sasa anaishi nchini Ugiriki amesema kutokana na yale aliyopitia, safari ngumu ya kunusurika kifo na sasa angalau anaona mwanga mwishoni mwa tanuru, amejizatiti kusaka elimu na ufahamu ili hatimaye asaidie watoto wengine kwa kuwa anafahamu maana ya maisha
Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limesema ukosefu wa ajira endelevu na makazi salama kutokana na janga la corona au COVID-19 na athari zake za kiuchumi vimewaacha maelfu ya wafanyak
Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limesema ukosefu wa ajira endelevu na makazi salama kutokana na janga la corona au COVID-19 na athari zake za kiuchumi vimewaacha maelfu ya wafanyakazi wahamiaji nchini Lebanon katrika hatari kubwa ya usafirishaji haramu wa binadamu na ukatili.