Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

12 MACHI 2024

12 MACHI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini India ambapo wahandisi wa usanifu majengo waliodhamiria kujenga mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kupunguza changamoto ya hewa ukaa katika sekta ya ujenzi kwa kutumia matofali ya matope. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani kama zifuatazo. 

  1. Meli iliyosheheni misaada ya kibinadamu imeanza safari yake kutoka Cyprus kuelekea Gaza ikiwa na shehena ya tani 200 za misaada ya kuokoa maisha kwa ajili ya wananchi wa Gaza.
  2. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP hii leo linaonya kuwa litalazimika kusitisha misaada ya kuokoa maisha nchini Chad ifikapo mwezi ujao wa Aprili iwapo litakosa ufadhili wa haraka kwa ajili ya kusaidia wakimbizi. 
  3. Na mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68, ukiendelea hapa jijini New York Marekani hii leo kutakuwa na mikutano ya kujadili mambo mbalimbali ikiwemo hali ya wanawake nchini Afghanistan, kuziba pengo la kujinsia kwenye elimu, athari za umaskini na uhalifu katika huduma ya utoaji mimba pamoja na mkutano wa kuangalia jinsi mabunge yanayozingatia jinsia katika kuendeleza usawa wa kijinsia ili kumaliza umaskini.
  4. Katika mashinani tunakuletea ujumbe wa Marynsia Mangu, kijana kutoka Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la Success Hands Tanzania anayeshiriki mkutano wa 68 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW68 hapa New York, Marekani akielezea matarajio yake kwenye mkutano huu.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'6"