Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

11 MACHI 2024

11 MACHI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu mwezi mktukufu wa Ramadhan, na uwezeshaji wa wanawake wakulima nchini Malawai. Makala na mashinani tunakupeleka nchini Kenya, kulikoni? 

  1. Leo ni mwanzo wa mwezi mktukufu wa Ramadhan ambapo Waislamu kote duniani husherehekea na kuchagiza tunu za amani, maridhiano na mshikamano lakini uhasama unaendelea hususani sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Gaza ambako mauaji , na mashambulizi hayajakoma amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani hii leo.
  2. Nchini Malawi Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya Kilimo IFAD unatekeleza mradi wa kuwasaidia wanawake wa vijijini kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia na sasa wananachi wanafaidi matunda yake. 
  3. Makala inatupeleka katika shule ya Salama iliyo katika eneo la Huruma karibu na mtaa wa mabanda wa Mathare jijini Nairobi Kenya hivi karibuni imeanza programu ya mlo shuleni kupitia mradi wa kampuni ya ‘Food for Education”. Hatua hiyo imenfa idadi ya wanafunzi wanaosoma shule hiyo kuongezeka kutoka 1, 900 hadi 2,300. Mlo shuleni ni moja ya masuala ambayo yanapigiwa debe kubwa na Umoja wa Mataifa sio tu kwa sababu ya kuhakikisha lishe bora kwa mamia ya maelfu ya wanafunzi ambao wengi hawawezi kupata mlo nyumbani bali pia kuongeza idadi ya watoto wanaohudhuria masomo.
  4. Na mashinanitunasalia nchini Kenya kumulika jinsi mradi wa FAO umemwezesha msichana mwenye ulemavu kuondokana na msongo wa mawazo na kisha kujikwamua kiuchumi.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

Audio Credit
Flora Nducha
Sauti
13'28"