Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB, cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, kimefikia makubaliano na wakazi wa kata za Ngadi na Matembo jimboni Kivu Kaskazini ya kutekeleza mradi wa taa za barabarani kama njia mojawapo ya kuimarisha usalama kwenye eneo hilo lililogubikwa na vikundi vilivyojihami vinavyoshambulia raia.