Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

29 FEBRUARI 2024

29 FEBRUARI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia siku ya mwisho ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia kipindi cha mpito nchini Sudan (UNITAMS), na afya kwa wakimbizi wa DRC jimboni Kivu Kaskazini.   Makala na mashinani tunaangazia mkutano huo wa Baraza la mazingira duniani UNEA6 leo ikiwa ni siku yake ya 4.

  1. Ikiwa leo ndio siku ya mwisho ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia kipindi cha mpito nchini Sudan (UNITAMS), Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema pamoja na kwamba UNITAMS inaondoka Sudan lakini Umoja wa Mataifa hauondoki nchini humo na unaendelea kujitolea kwa dhati kutoa usaidizi wa kibinadamu wa kuokoa maisha na kusaidia watu wa Sudan katika matarajio yao ya mustakabali wenye amani na usalama.
  2. Nchini Jamhuri ya kidemokrasia kongo DRC Jimboni kivu kaskazini zaidi ya wakimbizi milioni 2.5 wanaishi katika kambi za wakimbizi ambazo zina hali mbaya ambayo ni tishio kwa afya zao. Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO linatoa usaidizi kwa wakimbizi hao. 
  3. Makala tunakupeleka jijini Nairobi, Kenya kunakoendelea mkutano huo wa Baraza la mazingira duniani UNEA6 leo ikiwa ni siku yake ya 4. Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Nairobi UNIS amezungumza na vijana wawili wanaoshiriki mkutano huo ambao ni wanaharakati wa mazingira wanaotumia sayansi na sanaa kuleta mabadiliko katika jamii na pia ndio waliobuni sanaa ya jukwaa la mbao ambalo limewekwa kwenye lango la UNEA6 likipewa jina “Get your Seat at the Table.”
  4. Na mashinani tunasalia nchini Kenya katika mkutano wa sita wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEA6 kusikia mchango wa vijana katika kusongesha Malengo ya maendeleo endelevu.

Mwenyeji wako ni Evarist Mapesa, karibu!

Audio Credit
Evarist Mapesa
Sauti
11'10"