Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

27 FEBRUARI 2024

27 FEBRUARI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia hatari ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza na wakimbizi wa Sudan wanaovuka mpaka kuelekea Sudan Kusini. Makala tunakuletea majibu ya Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Dennis Francis alipohojiwa na UNTV kandoni mwa Kikao cha 55 cha Baraza la Haki za Binadamu kinachoendelea jijini Geneva Uswisi na mashinani tunakupeleka nchini Afghanistan, kulikoni?  

  1. Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani WHO na la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR leo yameonya kwamba athari zinazoletwa na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile saratani, magonjywa na mfumo wa hewa na kisukari kwa maisha ya watu duniani ni kubwa huku yakiwa ni chanzo cha asilimia 75 ya vifo vyote.
  2. Wananchi waliokimbia makazi yao kutokana na vita inayoendelea nchini Sudan wanasaidiwa nchini Sudan Kusini na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM ambalo limeeleza zaidi ya watu nusu milioni wamevuka mpaka na kuingia eneo la Renk na sasa wanawapatia usaidizi wa usafiri ili kufika kwenye maeneo watakayopata usaidizi. 
  3. Katika makala Anold Kayanda anaangazia majibu ya Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Dennis Francis alipohojiwa na UNTV kandoni mwa Kikao cha 55 cha Baraza la Haki za Binadamu kinachoendelea jijini Geneva Uswisi. Pamoja na mambo mengine Balozi Francis amesema Umoja wa Mataifa "sio tatizo" bali tatizo linatokana na kwamba baadhi ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanahisi wanaweza kukiuka mkataba wa Umoja wa Mataifa na  sheria za kimataifa watakavyo.
  4. Na mashinani tutaelekea nchini Afghanistan kusikia jinsi UNICEF ilivyorejesha huduma za afya, matibabu na mafunzo kwa wataalam ili kuwafikia watoto na wanawake popote walipo.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
11'13"