Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

26 FEBRUARI 2024

26 FEBRUARI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa sita wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA6 jijini Nairobi, na mradi wa kusaidia watoto na vijana ambao walikuwa na changamoto ya masikio na kuongea nchini Rwanda. Makala tunasalia nchin Kenya na mashinani ukanda wa Gaza, kuikoni?

  1. Mkutano wa sita wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA6 leo umefungua pazia katika Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo jijini Nairobi, nchini Kenya. Mkutano huo utakaodumu kwa siku tano unahudhuriwa na washiriki zaidi ya 6000 ikiwa ni pamoja na viongozi wa Mazingira duniani, asasi za kiraia, wataalamu wa Mazingira, maofisa waserikali za mitaa, wakulima, vyama vinavyowakilisha wafanyakazi, jamii zilizoachwa nyuma pamoja na maofisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa.
  2. Kupitia mradi wa "Winsiga Ndumva", maneno ya lugha ya Kinyarwanda yanayomaanisha "Usiniache nyuma, ninaweza kusikia”, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na wadau wake ikiwemo Wizara ya Afya nchini Rwanda limebadilisha maisha ya watoto wengi na vijana ambao walikuwa na changamoto ya masikio na kuongea kwakuwapatia vifaa maalumu vya kupachika masikioni ili kusaidia masikio kufanya kazi yake ipasavyo. 
  3. Makala inatupeleka kaunti ya Samburu nchini kenya kuona namna ngamia wanavyoboresha maisha ya wanawake na jamii kwa ujumla.
  4. Na mashinani inatupeleka katika ukanda wa Gaza ambapo ongezeko kubwa la utapiamlo miongoni mwa watoto na wanawake wajawazito na wanaonyonyesha ni tishio kubwa kwa afya zao. Shirika la Mpango wa chakula Duniani, WFP linahaha kuwasambazia lishe yenye virutubisho.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
9'57"