Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

23 JANUARI 2024

23 JANUARI 2024

Pakua

Hii leo jaridani mada kwa kina, ambapo katika mchakato wa kuleta mabadiliko kwa kuwezesha wanaojifunza kupata ufahamu muhimu, maadili, mienendo, stadi na tabia na hivyo wawe wachagizaji wa amani kwenye jamii zao, tnakupeleka katika makazi ya wakimbizi nchini Uganda kuona ni kwa vipi mchakato huo unafanyika. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani.

  1. shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeonya kwamba watu 570,000 wanakabiliwa na janga kubwa la njaa kutokana na kuendelea kwa mapigano makali, wahudumu wa misaada kunyimwa fursa ya kuwafikia wenye uhitaji na kukatwa kwa mawasiliano, sababu ambazo pia zimeathiri uwezo wa shirika hilo kufikisha na kusambaza msaada kwa usalama kwa maelfu ya watu. Hivyo limetoa wito wa kuongezwa haraka fursa za usambazaji na ufikishaji wa misaada ya kibinadamu. 
  2. Kwingineko wito wa kuchukuliwa hatua za haraka kushughulikia ongezeko kubwa la vifo vya wakimbizi wa Rohingya baharini umetolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Kwa mujibu wa shirika hilo wakimbizi wa Rohngya 569 walipoteza maisha au kupotea walipotumia safari hatari za boti katika bahari ya Andaman na Ghuba ya Bengal mwaka 2023, hiyo ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya waliopoteza Maisha tangu mwaka 2014.
  3. Na huko Ukraine Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu wa nchi hiyo Denise Brown amelaani vikali wimbi jipya la mashambulizi ya anga ya Urusi dhidi ya miji iliyo na watu wengi nchini Ukraine. 
  4. Mashinani tutaelekea katika ukanda wa Gaza kusikia ujumbe kuhusu harakati za chanjo kwa watoto ambao tayari wamekumbwa na changamoto ya vita.      

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
12'37"