nishati endelevu

Mjadala wa aina yake wa ngazi ya juu kuhusu nishati unaofanyika Ijumaa hii, haujapata kutokea kwa takribani miaka 40  

Sambamba na azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa namba 74/225, Katibu Mkuu Ijumaa hii ya tarehe 24 Septemba ameandaa mjadala wa ngazi ya juu wa Nishati wakati huu wa Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA76 ili kuharakisha utekelezaji wa lengo namba 7 la maendeleo endelevu linalohusiana na nishati endelevu.  

Nishati ya Ethanol itakuwa mbadala wa mkaa-UNIDO Tanzania

Nishati ya ‘Ethanol’ inayotokana na masalia ya vitu mbalimbali kwa mfano mazao kama miwa, mahindi, viazi na hata ngano ni moja ya suluhisho linaloonekana kuwa mjarabu kwa uharibifu wa mazingira unaosababishwa na matumizi ya nishati kama mkaa.

Sauti -
3'43"

UNHCR leo imezindua mkakati wa kimataifa wa nishati endelevu 

Kwa kutambua ongezeko la changamoto za mabadiliko ya tabianchi na kuinua uwezo wa wakimbizi katika kupata fursa za nishati salama na endelevu, huku likipunguza athari katka ka mazingira, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limezindua mkakati wa kimataifa wa miaka minne kwa ajili ya nishati endelevu. 

Kampeni kuhusu nishati endelevu yashika kasi, Uganda

Nishati endelevu ni suala ambalo linatathminiwa katika juhudi za kupambana na uchafuzi wa mazingira na athari zake duniani kote. Hili pia linapigiwa chepuo katika lengo namba saba la malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa SDGs au agenda ya 2030.

Sauti -
3'48"

Joto latesa zaidi ya watu bilioni moja duniani, maskini taabani- Ripoti

Zaidi ya watu bilioni moja duniani wako hatarini kutokana na viwango vya juu vya joto kali na kukosa mbinu za kukabiliana navyo.