Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

27 MACHI 2023

27 MACHI 2023

Pakua

Jaridani leo tunaangazia Afya na elimu. Makala tunasalia hapa makao makuu kufuatilia kazi ya vijana katika kutafuta suluhisho endelevu la upatikanaji wa maji barani Afrika na mashinani tutaelekeanchini Tanzania, kulikoni?

  1. Mashirika manne ya kimataifa yakiwemo matatu ya Umoja wa Mataifa yanayotekeleza mpango wa kimataifa wa ‘Afya Moja’ au ‘One Health’, hii leo yametoa wito wa ushirikiano wa kimataifa ili kujenga mifumo imara ya afya kufanikisha kukabiliana na changamoto ngumu za kiafya zinazoukabili ulimwengu.
  2. Ukame unaoendelea Pembe ya Afrika umeathiri shule zaidi ya 100 katika kaunti ya Turkana Kenya na kusababisha watoto wengi kuacha shule. Sasa shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Kenya kwa ushirikiano na mradi wa Educate a child wanaisaidia serikali kusajili watoto shuleni na kuhakikisha waliosajiliwa wanasalia shuleni.
  3. Katika makala Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anazungumza na Lauriel Kivuyo, Mwanaharakati kijana huyu wa tabianchi kutoka Tanzania ambaye alishiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maji.
  4. Na katika mashinani tunaelekea nchini Tanzania kusikiliza shairi ambalo limeandikwa na kukaririwa kwa ajili ya kutetea haki za watoto hususani wasichana.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
13'23"