Teknolojia

Vijana waunda roboti ya kusaidia watu wenye ulemavu

Hawana kisomo cha chuo kuu lakini ujuzi wao katika masuala ya teknolojia ya kuunda roboti inayoweza kusoma na kuelewa anachofikria mwanadamu na ni uvumbuzi ambao umewashangaza wengi.

Sauti -
4'35"

25 MACHI 2021

Katika Jarida la Habari za UN hii leo Grace Kaneiya anakuletea

Sauti -
13'5"

Watunga sera chukueni hatua nchi zinufaike na TEHAMA- UNCTAD

Baadhi ya mataifa yanayoendelea yanaonesha uwezo wa kutumia na kuchukua teknolojia mpya ikilinganishwa na vipimo vya pato la kitaifa lakini nyingi bado zinasalia nyuma, imesema ripoti mpya ya Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD ya mwaka 2021 ambayo imetolewa leo Februari 2

Sauti -
2'43"

25 Februari 2021

Jaridani hii leo Flora Nducha anamulika teknolojia na hatua ambazo serikali zinapaswa kuchukuliwa ili ziweze kunufaisha kila mtu na zilete maendeleo ya watu. Watunga sera wakiwemo wabunge wana jukumu lao, ni kutoka UNCTAD.

Sauti -

Nchi kadhaa zinazoendelea zinafanya vizuri katika matumizi ya teknolojia mpya lakini nyingi zasalia nyuma-UNCTAD Ripoti 

Baadhi ya mataifa yanayoendelea yanaonesha uwezo wa kutumia na kuchukua teknolojia mpya ikilinganishwa na vipimo vya pato la kitaifa lakini nyingi bado zinasalia nyuma, imesema ripoti mpya ya Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD ya mwaka 2021 ambayo imetolewa leo Februari 25 mjini Geneva Uswisi. 

ATM kuanza kutumika kugawa chakula kwa wahitaji Afrika Mashariki na Kati- WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP hivi sasa limegeukia njia mbalimbali bunifu katika mnyororo wake wa usambazaji Afrika Mashariki na Kati kwa lengo la kuokoa na kubadili haraka maisha ya mamilioni ya watu wanaohitaji msaada. Je ni mbinu gani hizo ?.

Sasa hatuonji tena maji, tunatumia simu za kiganjani- Wakulima wa mpunga Vietnam

Nchini Vietnam, mfuko wa maendeleo ya Umoja wa Mataifa, IFAD umesaidia wakulima kuondokana na tabia ya kuonja maji ya umwagiliaji ili kutambua kiwango cha chumvi na badala yake sasa wanatumia teknolojia ya simu ya kiganjani ili kuongeza mavuno ya mpunga. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Sauti -
2'49"

Vijana Kenya wavumbua apu ya simu itakayosaidia katika upandaji miti

Miti huchangia kwa kiwango kikubwa katika kutunza mazingira kwa kuzuia kuenea majangwa kupitia kuleta mvua na pia kutunza vyanzo vya maji ardhini. Kwa upande wa uchumi hali kadhalika, miti ina manufaa kama vile mbao.

Sauti -
3'46"

Tutahakikisha wanafunzi walio nje ya shule wanasoma wakati wa COVID-19:UNESCO/ITU

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO limezindua muungano wa elimu wa kimataifa ili kuhakikisha wanafunzi walio nje ya shule kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19 wanasoma kupitia teknolojia

Shule ya kwanza ya mafunzo ya ndege zisizo na rubani na takwimu yafunguliwa Afrika-UNICEF

Shule ya kwanza ya mafunzo kuhusu ndege zinazoruka bila rubani (Drone) na takwimu, ADDA imefunguliwa Lilongwe, nchini Malawi Januari 13 mwaka 2020 limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.