Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

29 OKTOBA 2019

29 OKTOBA 2019

Pakua

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Arnold Kayanda anakuletea

-Mafuriko yameighubika Pembe ya Afrika, shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA na wadau wengine wanahaha kuwasaidia maelfu ya waathirika Sudan kusini, Somalia na Ethiopia.

-Jukumu la wanawake walinda amani kwenye mizozo katika operesheni za Umoja wa Mataifa ni zaidi ya kubeba mtutu amesema balozi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa

-Milima imeelezwa kuwa na mchango mkubwa katika kujenga mnepo dhidi ya mabadiliko ya taibianchi katika mkutano wa kimataifa ulioitishwa na shirika la utabiri wa hali ya hewa WMO mjini Cairo Misri.

-Makala yetu leo inatupeleka Turkana Kenya tutasikia kutoka kwa manusura wa ndoa za mapema

-Na mashinani tunabisha hodi Kenya kwake  waziri wa afya , Sicily Kariuki akitoa wito wake kwamba siku zote kinga ni bora kuliko tiba

Audio Credit
UN News/Arnold Kayanda
Audio Duration
12'14"