Mfumo mpya wa usalama barabani utasaidia kuokoa maisha ya mamilioni UNECE
Tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi barani Ulaya UNECE, imeanzishia mfumo mpya utakao dhibiti na kutoa taadhari ya matukio barabarani kwa watumiaji vyombo vya usafiri wakati wa majanga au ajali.
UNECE imesema mfumo huo mpya uitwao AECS umeandaliwa kwajili ya vyombo vya usafri lengo likiwa ni kutoa taadhari za matukio ya dharura kama vile kwa idara ya zimamoto au mgari ya kubeba wagonjwa wakati wa ajali au majanga mengine na pia kutoa ramani ya eneo la tukio ikiwa ni njia moja wapo ya kuokoa maisha kwa kutumia teknolojia mpya
Mfumo wa AECS uliopitishwa na bodi ya Umoja wa Mataifa inayosimamia sheria za usafiri wa magari namba WP.29 ikiwa ni moja ya binu zinazowezesha teknolojia mpya katika uboreshaji wa usalama barabarani.
Sheria hii mpya inatarajiwa kuanza kazi mwezi Juni mwaka 2018 kwa nchi zitakazoweza kuitumia chini ya kifungu cha sheria ya mkataba wa 1958, katika kusaidia juhudi za kimataifa za kuboresha usalama barabarani.