WFP yapokea dola milioni 5 toka HNA, kusaidia wakimbizi Syria
Shirika la mpango wa chakula duniani WFP leo limetangaza kupokea dola milioni 5 kutoka shirika la misaada ya kibinadamu la China HNA ili kuwasaidia wakimbizi wa Syiria walioko Uturuki, na Lebanon kwa miaka mitatu ijayo katika ubia mpya.
Ushirikiano huu kati ya WFP na HNA ulitiwa saini baina ya Mkurungezi mkuu wa WFP David Beasley na makamu mwenyeki wa HNA Li Xianhua mjini Beinjing China.
Bw Beasley amesema msaada huu toka HNA unazidi kuimarisha nafasi ya serikali ya watu wa China kwa ulimimwengu katika kutoa misaada ya kibinadamu na hususani kuhakikisha watu walioko katika mazingira magumu kama wakimbizi wa Syria wanapatia usaidizi.
Aidha Bwana Beasley ameushukuru uongonzi mzima wa HNA kwa msaada huo ambao utatumika kusaidia katika program za shule za watoto wakimbizi wa ndani na walioko katika maeneo tofauti huko Lebanon na Utukuri.
Ushirikiano baina ya WFP na HNA ulianza mwaka 2013 amabapo HNA ilitoa mchango dola milioni 1.6 ili kusaidia chakula cha shule kwa karibu watoto 4,000 huko Ghana na sehemu nyigine magharibi mwa Afrika.