Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hewa chafuzi kutoka kwenye kilimo itaendelea kwa mwiba kwa tabianchi- FAO

Hewa chafuzi kutoka kwenye kilimo itaendelea kwa mwiba kwa tabianchi- FAO

Pakua

Shirika la chakula na kilimo, FAO limesema kiwango cha hewa chafuzi kutoka katika shughuli za kilimo kitaongezeka siku zijazo na kuleta madhara katika tabianchi.

Mkurugenzi Mkuu wa FAO José Graziano da Silva amesema hayo leo huko Bonn, Ujerumani kwenye mkutano wa 23 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP23.

Kwa mantiki hiyo amesisitiza umuhimu wa kuzingatia mbinu bora za kilimo, usafiri na ulaji wa chakula akisema bila kufanya hivyo maisha ya mamilioni ya watu yako hatarini.

Bwana da Silva amesema ingawa kuna changamoto katika kudhibiti mabadiliko ya tabianchi, vikwazo hivyo visirudishe nyuma ari ya kutekeleza mbinu sahihi ya kulinda tabianchi.

Mathalani amesema haitoshi tu kubadili mbinu za kuzalisha chakula, bali mfumo mzima lazima ubadilike kuanzia uzalishaji, uchakataji hadi ulaji wa vyakula mijini na vijijini.

Kwa mantiki hiyo ametaka suala la mabadiliko ya tabianchi pamoja na umaskini na njaa vichukuliwe hatua kwa pamoja.

Photo Credit
Kilimo, misitu na shughuli nyingine za matumizi ya ardhi hutoa tani zaidi ya bilioni 10 za gesi chafuzi. Picha: FAO / Daniel Hayduk