Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viua vijasumu ni hazima tutumie kwa uangalifu- WHO

Viua vijasumu ni hazima tutumie kwa uangalifu- WHO

Pakua

Wiki ya kuhamasisha umma kuhusu usugu wa viua vijasumu imeanza leo ambapo shirika la  afya ulimwenguni WHO linataka jamii ifahamu umuhimu wa kupunguza matumizi ya dawa hizo kwa wanyama na binadamu kama njia mojawapo ya kuepusha matumizi yasiyo sahihi na yasiyo ya lazima.

Kupitia wavuti wake, WHO inasema usugu husababisha dawa hizo kushindwa kufanya kazi yake pindi mnyama au binadamu anapokumbwa na maradhi na hivyo kusababisha kifo.

Kwa hali hiyo WHO inasema tiba za kawaida zinashindikana na kusababisha magonjwa kuenea kwa wanyama na binadamu.

Nats

Katika video hii inayotumia vikaragosi, WHO inaonyesha ni kwa jinsi gani magonjwa yanaenea na matumizi yasiyo sahihi ya viuvijasumu yanavyosababisha  usugu na vijidudu au vijiumbe maradhi kusalia hai mwilini mwa binadamu au mnyama.

Kwa mantiki hiyo WHO inatoa ujumbe kupitia picha, video na sauti ikitaka kila mtu azuie matumizi ya viua vijasumu kwa kuepusha maambukizi ya magonjwa.

Mosi kwa kuosha mikono kabla ya kuandaa chakula, kuziba pua pindi mtu anapopiga chafya au kukohoa, bila kusahau ngono salam na kuhakikisha kila mtu anapata chanjo sahihi kwa wakati muafaka.

Hata hivyo WHO inasema iwapo mtu anakuwa mgonjwa, ni lazima kusaka ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa aina ya viua vijasumu au antibayotiki.

Ujumbe wa WHO ni kwamba viua vijasumu ni hazina hivyo tutumie kwa uangalifu.

Photo Credit
Pata ushauri wa daktari au mhudumu wa afya kabla ya kutumia Viua vijasumu. Picha: WHO