Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP kuanzisha mafunzo ya kimtandao kuhusu ulinzi wa mazingira ya asili

UNEP kuanzisha mafunzo ya kimtandao kuhusu ulinzi wa mazingira ya asili

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP limeanzisha mafunzo ya kimtandao kuhusu  ulinzi wa mazingira  ikiwa ni hatua muhimu katika kukomesha  migogoro juu ya rasilimali za asili  ambayo ni changamoto kubwa katika siasa ya karne ya 21 na kuhatarisha usalama wa binadamu.

Hiyo ni mujibu wa Erik Solheim said ambaye ni mkurungezi wa UNEP katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuzuia vita ambavyo ni sababu kubwa na uharibifu wa mazingira duniani hapo jana tarehe 5 novemba.

Bwana Erik amesema   asilimia 40 ya migogoro yote katika  kipindi cha miaka 65 iliyopita imechanigia sana uharibifu  wa rasilimali za asili. Amesema tangu mwaka 1989, makundi ya wanamgambo zaidi  ya 35 yamefadhiliwa na mapato kutokana na rasilimali zitokazo kwenye maeneo yenye  migogoro.

Aidha UNEP na baadhi ya vyo vikuu kama chuo Kikuu cha Columbia, chuo kikuu cha Duke, na Chuo Kikuu cha California huko Irvine wameazisha  kozi mpya ya kimtandao ya wiki 10 yenye lengo la  kutoa mafunzo kuhusu  usalama wa mazingira  na rasilimali za asili  na kudumisha amani katika  maeneo yenye migogoro.

Photo Credit
Uharibifu wa wa mazingira. Picha: UNEP