Maelfu ya raia wa Cameroon wakimbilia nchini Nigeria
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi , UNHCR, pamoja na mamlaka ya Kusini Mashariki mwa Nigeria, wamepokea maelfu ya wakimbizi kutoka Cameroon waliokimbilia nchini humo kutafuta hifadhi na usalama, baada ya uhasama mpya uliozuka mwezi oktoba katika eneo linazumgumza kiingereza Cameroon.
UNHCR na tume ya taifa ya Wakimbizi (NCFRMI) wanasema hadi sasa wameandikisha wakimbizi 2,000 kwa msaada wa wananchi wa eneo hilo la kusini Mashariki mwa Nigeria. Wamesema wakimbizi wengine zaidi wanasubiri usajili, na wengi bado wapo mafichoni katika misitu ya Camerron wakati wanajaribu kuvuka mpaka.
Aidha UNHCR na serikali ya Nigeria wamesema wapo katika mchakato wa kuaanda eneo jipya la kuwahifadhi wakimbizi hao. Pia wametoa misaada mbalimbali ikiwa ni pamoja na magodoro, mablanketi, vyandarua, vifaa vya kupikia na kujisafi, na tani 40 za chakula.
UNHCR imesema itaendelea kushirikiana na serikali ya Nigeria na mashirika ya kibinadamu katika kutoa huduma kwa wakimbizi hao, wakiwa na hofu kwamba idadi ya wakimbizi hao inaweza kuongezeka kufikia 40,000 kutokana la taarifa kutoka mashinani ambako migogoro inaendelea.
Nigeria na Cameroon tayari wanakabiliwa na janga la boko Haramu katika eneo la Ziwa Chad ambalo tayari limewaathriri watu zaidi milion 2.5