Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume ya uchunguzi wa haki Burundi yaongezwa mwaka mmoja:UM

Tume ya uchunguzi wa haki Burundi yaongezwa mwaka mmoja:UM

Pakua

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa leo limehitimisha kikao chake mjini Geneva Uswis kwa kupiga kura na kupitisha maazimio matano muhimu likiwemo la haki za binadamu nchini Burundi.

Azimio la kuongeza muda wa majukumu ya tume ya uchunguzi wa ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi imepita kwa kura 22 zilizounga mkono, 11 zilipinga na wajumbe 14 hawakupiga kura kabisa.

Azimio hilo limetoa mwaka mmoja zaidi kwa tume ya uchunguzi na kutaka kutumwa haraka wataalamu watatu wa haki za binadamu kwenda kukusanya taarifa, kushirikiana na serika ya Burundi na kufichua ukweli ili wahusika wa ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo wawajibishwe.

Pia maazimio mengine yaliyopitishwa na kikao hichoni pamoja na la kuhusu Syria ambapo baraza litaitisha mjadala wa ngazi ya juu kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu za watoto unaoendelea nchini Syria. Pia azimio kuhusu masuala ya haki, la hukumu ya kifo na la pingamizi katika huduma za kijeshi.

Photo Credit
Kikao cha Baraza la Haki za Binadamu. Picha: Umoja wa Mataifa/ Jean-Marc Ferré