Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili zaidi wahitaji kwa wakazi wa bonde la ziwa Chad- Lowcock

Ufadhili zaidi wahitaji kwa wakazi wa bonde la ziwa Chad- Lowcock

Pakua

Ufadhili zaidi unahitajika ili tuweze kuendelea kutoa misaada muhimu ya kibinadamu kwenye bonde la ziwa Chad, amesema  mkuu mpya wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA Mark Lowcock akizungumza na waandishi wa habari jijini New York kufuatia ziara yake kwenye eneo hilo.

Ziara hiyo ililenga kupazia sauti madhila yanayokumba zaidi ya watu milioni 17 kwenye eneo hilo ambapo amesema alitiwa moyo na ahadi za ufadhili zilizotolewa na nchi mbali mbali hivi karibuni za takriban dola milioni 120.

Amesema ahadi hizo ni pamoja na dola milioni 100 kwa ajili ya shirika la mpango wa chakula duniani, WFP na kutoka kwa Marekani pia ahadi ya Nigeria kwa ajili ya wakimbizi wa ndani walioko Kaskazini Mashariki mwa Nigeria kufikia mwaka 2018.

Bwana Lowcock amesema janga la maeneo ya bonde la ziwa Chad ni tata kwani kuna changamoto za ukosefu wa usalama, mabadiliko ya tabianchi, umaskini uliokithiri na uongozi pungufu lakini kusonga mbele…

(Sauti ya Lowcock)

“Tukiongozwa na nchi zinazowahifadhi wakimbizi tunahitaji kuhakikisha misaada ya kibinadamu, pili tunahitaji ulinzi bora kwa raia, na tatu tunahitaji kuona jitihada katika amani na maendeleo hizo ndizo hatua muafaka kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya maeneo hayo.”

Photo Credit
Mkuu mpya wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA,Mark Lowcock alipokuwa Ziarani CHAD. Picha: UM