Skip to main content

Vyombo vya habari vyazidi kuminywa nchini Misri

Vyombo vya habari vyazidi kuminywa nchini Misri

Pakua

Wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa wameeleza wasiwasi wao juu ya vitendo vya serikali ya Misri kubinya uhuru wa kujieleza wa vyombo vya habari nchini humo.

Wataalamu hao ni David Kaye ambaye ni wa masuala ya uhuru wa kujieleza, na Fionnuala Ní Aloáin anayejikita katika kupambana na ugaidi.

Katika taarifa yao, wataalamu hao wameshtushwa na ripoti ya orodha za tovuti ya vyombo vya habari zilizofungwa na mamlaka husika kupitia shirika la habari la serikali MENA,  kwa vigezo vya kueneza uongo' na kuunga mkono ugaidi.

Wataalamu hao wamesema kwamba  hali ya uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza  nchini Misri imekuwa katika mgogoro kwa miaka kadhaa na sasa imechukua hatua nyingine, ikiwa ni pamoja na kuzuia kinyume cha sheria na unyanyasaji wa waandishi wa habari .

Tovuti  zilizofungiwa ni pamoja na zile za vyombo vya  habari vya MadaMasr, RASSD, Al Watan na Huffpost Arabi pamoja na tovuti maarufu  za mashirika ya haki za binadamu kama vile waandishi bila mipaka.

Photo Credit
IRIN/Amr Emam (file)