Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wapaswa kuchangamkia fursa: Kijana Fatma

Vijana wapaswa kuchangamkia fursa: Kijana Fatma

Pakua

Uthubutu na kusaka fursa badala ya kusubiri miujiza ni nyenzo muhimu ya mafanikio kwa vijana, amesema Fatma Said Ahmed, Mwanzilishi wa taasisi ya StandforHumanity na pia mshiriki wa mwaka  2016 wa kundi la viongozi vijana la Michael Johnson.

Katika mahojiano na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, nchini Tanzania, Fatma ambaye hujihusisha na masuala ya vijana na maendeleo, amesema muhimu zaidi ni jamii kupata elimu kwa mujibu wa lengo namba nne la maendeleo endelevu SDGs, linalotaka elimu kwa wote.

(Sauti Fatma)

Amesema hatua ambazo vijana wanapaswa kuchukua ni.

(Sauti Fatma)

Photo Credit
Fatma Said Ahmed (kulia) akihojiwa na Stella Vuzo wa UNIC Dar es Salaam. (Picha:UNIC Dar)