Skip to main content

Simu za rununu zasaidia kutuma fedha kwa familia zilizoathirika na vita Iraq: FAO

Simu za rununu zasaidia kutuma fedha kwa familia zilizoathirika na vita Iraq: FAO

Pakua

Familia nyingi za vijijini nchini Iraq sasa zinafaidika na njia salama na ya uhakika ya kupokea fedha, asante kwa teknolojia ya kutuma fedha kupitia simu za rununu, iliyoanza kutumiwa kwa mara ya kwanza na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO nchini humo kama sehemu ya mpango wa malipo ya fedha kwa kazi.

Mpango huo wenye lengo la kufufua tena kilimo, miundombinu na ardhi unafadhiliwa na serikali ya Ubeligijina utawasaidia watu 12,000 walioathirika na vita katika vijiji 30 kwenye majimbo ya Kirkuk, Anbar, Salah al-Din na Ninewa .

Mpango huo kwa mujibu wa FAO utawasaidia sana wakulima na kuwawezesha kuanza upya au kupanua shughuli zao za kilimo, na kufufua miundombinu na kutoa fursa za ukulima kwa maelfu ya watu waliotawanywa na vita ambao sasa wanarejea nyumbani.

Washiriki wakubwa kwenye mpango huo wa kupokea fedha katika familia ni wanawake ambao ndio walezi wa familia na watu wenye ulemavu.

FAO inasema teknolojia ya simu za rununu kutuma fedha ni rahisi, ya haraka na usalama na itakuwa mkombozi mkubwa kwa maelfu ya watu wasiojiweza.

Photo Credit
Simu za rununu zasaidia kutuma fedha kwa familia zilizoathirika na vita Iraq. Picha: FAO