Skip to main content

Mizozo yapandisha bei za vyakula: WFP

Mizozo yapandisha bei za vyakula: WFP

Pakua

Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani, WFP, imesema mizozo,  misukosuko na mifumo duni ya chakula ni kiini cha kupanda kwa gharama za chakula, wakati huu ambapo mahitaji ya kibinadamu yanaongezeka.

Kwa mfano, WFP, yenyewe inasema imeshuhudia kupanada kwa gharama zake za chakula  kutoka dola bilioni 2.2 kaitka mwaka 2009 hadi dola bilioni 5.3 ilipofika mwaka 2015.

Kanda za Masahriki na Afirka ya Kati, Mashariki ya Kati na Pembe ya Afrika, zinazoshuhudia mizozo mikubwa ndizo zinachukua asilimia 70 ya matumizi ya Shirika na Mpango wa chakula duniani, WFP.

Ripoti hiyo itwayo “Msaada wa chakula duniani, 2017: kuhifadhi chakula na kuona mbele”  inasema kuwa upatikanaji wa fursa ya misaada ya kibinadamu kufikia maeneo yenye mizozo, unaweza kupunguza gharama za chakula za WFP kwa takribani dola biilioni 1 kila mwaka.

Mkurugenzi Mtendaji wa WFP, David Beasly amesema, kutokomeza vita na mizozo ni ni jambo ambalo dunia inahitaji kupigania kuliko vyote  kama hatua muhimu katika juhudi za kuepuka njaa. Amesema duniani kote watu milioni 800 au mtu mmoja kati ya tisa ana lala bila kula na vita na mizozo inafanya kuwa vigumu sana kuwasaidia wanaohitaji msaada zaidi.

Photo Credit
Picha:WFP