Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana katika kampeni ya kutunza urithi wa kitamaduni

Vijana katika kampeni ya kutunza urithi wa kitamaduni

Pakua

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limekuwa likiendesha kampeni inayolenga kuwajumuisha vijana katika kulinda na kutunza maeneo ya urithi wa dunia.

Kampeni hii ilizinduliwa mnamo mwaka 2015, kufuatia mashambulizi dhidhi ya maeneo ya urithi wa kitamaduni, ikitoa wito kwa kila mmoja kupaza sauti dhidi ya itikadi kali, kwa kusheherekea maeneo, vitu na mila za kitamaduni zinazochangia uzuri na utajiri wa dunia. Katika makala ifuatayo, Joshua Mmali anatupeleka Ramallah, Palestina, ambako moja ya shughuli zinazohusiana na kampeni hiyo ilikuwa ikiendeshwa.

Photo Credit
Vijana wapalestina watumbuiza katika kulinda urithi wa kitamaduni. Picha: UNESCO/Video capture