Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna matumaini ya suluhu Burundi, nitaitisha mkutano wa dharura: Mkapa

Kuna matumaini ya suluhu Burundi, nitaitisha mkutano wa dharura: Mkapa

Pakua

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo Machi tisa, limejadili hali ya kiusalama nchini Burundi, ambapo imeelezwa kuwa usalama umeendelea kuzorota na hofu imetanda miongoni mwa raia.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kuhusu kuzuia migogoro Jamal Benomar, ameliambia baraza hilo kuwa ikiwa ni miaka miwili tangu kuzuka kwa mgogoro nchini humo, uhasama unaendelea miongoni mwa pande kinzani na kwamba.

( Sauti Benomar)

‘‘Warundi wengi wanaishi katika hofu,ikiwa ni matokeo ya kuenea kwa ukubwa ukandamizaji, na kuongezeka kwa vitisho vya kundi la vijana wanamgambo la chama tawala liitwalo Imbonerakure. Wajumbe wa vyama vya upinzani na wale wanaotizamwa kaam wapinzani, wanaripotiwa kwua wahanga wa utesaji, kuwekwa kizuizini na kutoweshwa.’’

Amesema kwamba cha kusikitisha zaidi ni kufungwa kwa milango ya ushirikiano dhidi ya Umoja wa Mataifa, kunakotekelezwa na mamlaka nchini humo.

Akilihutubia baraza hilo kwa njia ya video kutoka mjini Kampala nchini Uganda, Mwezeshaji wa mchakato wa suluhu ya mgogoro wa Burundi anayewakilisha Muungano wa Afrika AU, Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa amesema ana matumaini ya kufikiwa kwa muafaka baada ya kukutana na pande kinzani kwa nyakati tofauti.

Ameongeza kuwa hata hivyo kumekuwa na mkwamo katika kuzikutanisha pamoja pande kinzani kwa sababu mbalimbali na kwahiyo anachofikiria kufanya ni.

( Sauti Mkapa)

‘’Nitawataka wakuu wa nchi wakutane kwa dharura ili watoe msukumo  kwa pande hizo mbili, watambue umuhimu wa kuja pamoja na kujadili kwa dharura mambo hayo.’’

Photo Credit
Msuluhishi wa mgogoro wa Burundi anayewakilisha Muungano wa Afrika AU, Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa. Picha: UM/Video capture