Skip to main content

Kuzuia migogoro,ni kukuza maendeleo: Guterres

Kuzuia migogoro,ni kukuza maendeleo: Guterres

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo amezungumza katika kongamano la kimataifa la uchumi linaoendelea mjini Davos nchini Uswisi.

Katibu Mkuu ameiambia hadhira hiyo kuwa licha ya changamoto kadhaa za kiuchumi zainazoikabili dunia, kuzuia migogoro ni maendelo endelevu na jumuishi, akizitaka serikali, asasi za kiraia na wafanyabiashara kuhakikisha hilo linafanyika.

Guterres amesema wadau wa kibishara na maendeleoao wanapaswa kukumbuka kuwa wajibu wao sio biashara tu, bali pia kuainisha vipaumbele vyenye mitizamo yenye malengo ya kimataifa. Kuhusu utekelezaji wa malengo ya maendeleo enedelevu SDGs Katibu Mkuu amesema.

( Sauti Guterres)

‘‘Ni fursa kwa pande mbili, ya kukuza uwekezaji ambao unavutia sketa binafsi, sambamba na kuruhusu sekta binafsi kutekeleza wajibu wa msingi wa kuhakikisha malengo hayo yanatimia.’’

Amesema sekta binafi ni muhimu katika maendeleo kwa kuwa.

( Sauti Guterres)

‘‘Bila sekta binafsi hatutakuwa na ubunifu ambao ni muhimu. Bila sekta binafsi hatutaweza kuzalisha ajira mpya na mabadiliko endelevu kwa jamii ambayo inahitaji kuwezeshwa katika utekelezaji wa maendeleo endelevu.’’

Photo Credit
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza katika kongamano la kimataifa la uchumi linaoendelea mjini Davos nchini Uswisi. Picha: UM