Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mfululizo wa mashambulizi ya anga Syria

Ban alaani mfululizo wa mashambulizi ya anga Syria

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani mashambulizi ya anga katika siku za hivi karibuni chini Syria ambayo yameua na kusababisha ulemavu  kwa makumi ya raia wa Syria na kuiacha Allepo Mashariki bila hospitali.

Taarifa ya ofisi ya msemaji wa Katibu Mkuu imesema Ban pia amelaani makombora  aliyoyaita yasiyobagua, ambayo yameripotiwa katika jimbo la Allepo na mashariki mwa mji huo, ikiwamo mashambulizi dhidi ya shule ambayo yamedaiwa kuua watoto kadhaa.

Amezikumbusha pande zote kinzani kuwa kulenga raia na maiundombinu ya raia ni uhalifu wa kivita. Amezitaka pande hizo kusitisha mashambulizi hayo hima na kusisitiza kuwa wahusika wa mauaji hayo nchini Syria,  popote walipo siku moja lazima watafikishwa katika vyombo vya sheria.

Katibu Mkuu pia amezitaka pande hizo kuhakikisha uhuru wa raia kutembea na kuruhusu misaada ya kibinadamu.

Photo Credit
Moja ya mahsambulizi yaliyoharibu shule ya msingi nchini Syria.Picha na UNICEF/M. Abdulaziz