Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mameya wana jukumu muhimu katika ajenda mpya ya miji

Mameya wana jukumu muhimu katika ajenda mpya ya miji

Pakua

Mameya wa miji mikubwa ndio hasa watakaobeba bendera linapokuja suala la utekelezaji wa ajenda mpya ya miji iliyopitishwa kwenye mkutano wa tatu wa makazi yaani HABITAT 111 mjini Quito, Ecuador.

Huo ni mtazamo wa Mark Watts, mkurugenzi mtendaji wa kundi la masuala ya mabadiliko ya tabianchi liitwalo C-40 Climate Leadership Group, ambalo linawakilisha mameya 68 wa miji mikubwa duniani.

Akizungumza baada ya mkutano na waandishi wa habari na kundi la mameya wanaohudhuria mkutano huo wa HABITAT 111, amesema ajenda endelevu inayojadiliwa Quito ni muafaka kwa ajili ya kundi lake la mameya. Kwani mkutano huo ni muhimu sana kwa miji duniani

(SAUTI MARK WATTS)

“Ajenda endelevu kwenye mkutano huu ndio hasa ambacho mameya kote duniani wanataka kufanya au wanafanya katika miji yao. Tukichukulia mabadiliko ya tabia nchi kwa mfano ambayo yametamaklaki kwenye mkutano mahesabu yetu ni kwamba theluthi ya hewa ya canon iliyosalia itatumika katika miaka mine ijayo”

Hata hivyo amesema pamoja na juhudi zao changamoto kubwa ni fedha

(MARK CUT 2)

“Hawawezi kuwa na malengo makubwa kama wanavyotaka kwa sababu hiyo, lakini unachokiona ni kwamba mameya wanakuwa wabunifu na kutafuta njia ya kutekeleza mambo hata kama hawana fungu la kutosha kwa ajili yao, lakini kama tatizo hilo la fedha litatatuliwa itasaidia sana.”

Na akizungumzia ajenda hiyo mpya amesema

(MARK CUT 3)

“Ajenda hii ya miji inadhihirisha miaka 20 ya kazi kuhusu njia bora kwa miji kuendelea ambayo inajumuisha kwa pamoja kukabiliana na kutokuwepo usawa na kuhakikisha mazingira endelevu, hivyo nadhani ni muhimu lakini la msingi zaidi ni hatua zitakazochukuliwa baadaye."

Photo Credit
Mtazamo wa Mji wa Shanghai, China.(Picha:UM/Julius Mwelu/UN-Habitat)