Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upatikanaji wa mashine za kilimo ni muhimu kwa ajili ya uzalishaji na maisha ya vijijini

Upatikanaji wa mashine za kilimo ni muhimu kwa ajili ya uzalishaji na maisha ya vijijini

Pakua

Kulisha idadi kubwa ya watu inyoongezeka duniani kunahitaji uboreshaji wa hali ya juu katika usalishaji wa kilimo,mikakati na mbinu muafaka hususani barani Afrika, limesema shirika la kilimo na chakula FAO.

Ripoti ya shirika hilo imesema fursa ni lazima zitoe muongozo utakaozingatia mahitaji ya wakulima wadogowadogo na zisizohitaji mtazamo wa mapinduzi ya kijani yanayoambatana na matumizi makubwa ya dawa za kilimo na pembejeo zitakazoharibu na kutishia afya na rutuba ya mashamba.

Ripoti hiyo iitwayo “Zana za kilimo ni ufunguo kwa wakulima wadogowadogo Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara”inaeleza kwamba zana za kilimo au mashine katika karne hii ya 21 ni lazima ziende sanjari na uhifadhi wa mazingira, ziwe na faida kiuchumi, za gharama nafuu, zinazoweza kutumika popote, na zinaostahimili hali ya hewa inayobadilikabadilika.

Mkurugenzi msaidizi wa FAO Ren wang anasema bila shaka utumiaji wa mashine au zana muafaka ni muhimu katika uzalishaji wa kilimo Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, na kutaweza kubadili maisha ya mamilioni ya watu na uchumi vijijini.

Hivi sasa theluthi mbili ya zana za uzalishaji wa kilimo zinazotumika katika eneo hilo la Afrika ni msuli wa binadamu.

Photo Credit
Upatikanaji wa mashine za kilimo ni muhimu kwa ajili ya uzalishaji na maisha ya vijijini. Picha: FAO/Swiatoslaw Wojtkowiak