Aweka rehani familia ili kusaidia wakimbizi

Aweka rehani familia ili kusaidia wakimbizi

Pakua

Kila siku, maelfu ya wakimbizi na wahamiaji wanaweka maisha yao hatarini katika safari ya kuvuka bahari ya Mediteranea, wengi wao wakikimbia mateso na hali ngumu za maisha. Idadi kubwa wanatoka Syria, Iraq na Afghanistan wakipitia Ugiriki ili kufika nchi  nyingine za Ulaya.

Serikali ya Ugiriki imeshindwa kuwahudumia wakimbizi hao wote, lakini mashirika ya kibinadamu na watu binafsi wanajitolea kutoa usaidizi. Miongoni mwa watu binafsi ni Ali Abu Assad kutoka Denmark, yeye amefika Ugiriki ili kusaidia watu na ametumia pesa zake zote za akiba katika shughuli hizi, Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hiyo.

Photo Credit
Ali Abu Assad akiwa katika harakati za uokozi. (Picha:UNHCR/Videocapture)