Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutwa kucha tunapambana kuweka utulivu na amani Somalia; Kamanda AMISOM

Kutwa kucha tunapambana kuweka utulivu na amani Somalia; Kamanda AMISOM

Pakua

Kikosi cha Muungano wa Afrika nchini Somalia, AMISOM kinaendelea na harakati za ulinzi wa amani nchini humo licha ya changamoto zinazoendelea kuikumba Somalia. Mathalani kwa sasa AMISOM inajikita kudhibiti bandari zinazoshikiliwa, dhamira ikiwa ni kuwatenganisha wanamgambo wa AlShabaab na ngome zao kubwa wanakochota vifaa na kuendesha usajili wa wapiganaji. Hilo linaendelea wakati huu ambapo Kiongozi Mkuu wa Alshabab Ahmed Abdi «Godane» akiwa ameuawa kwa ushirikiano wa vikosi hivyo na Marekani. Je hali kwa sasa Somalia iko vipi? Basi mwandishi wetu wa Bujumbura, Burundi, Ramadhani Kibuga amezungumza na Kamanda Mkuu wa Vikosi vya AMISOM Luteni Generali Silas Ntigurigwa na hapa anaanza kwa kufafanua hali ilivyo.

Photo Credit
Kamanda Mkuu wa vikosi vya AMISOM Luteni Jenerali Silas Ntigurigwa. (Picha:AU UN IST)