Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

© UNICEF/Gwenn Dubourthoumieu

Ndoto za kuwa daktari au Mwalimu Mkuu kwa watoto hawa zitatimia?

Ijapokuwa ni wakimbizi wa ndani na wanaishi kwenye kituo cha kuhifadhi wakimbizi wa ndani cha Bushagara, mjini Goma, jimboni Kivu Kaskazini, mtoto Irene anataka kuwa daktari, na Christelle anataka kuwa Mwalimu Mkuu. Ingawa hivyo, elimu bado ni changamoto kubwa kwa watoto milioni 2.4 wakimbizi wa ndani nchini DRC hususan majimbo ya Kivu Kaskazini, Ituri na Kivu Kusini ambao wanahitaji elimu kwa haraka. Hoja ni iwapo ndoto zao hizo zitatimia au ndio zitapeperushwa na vita inayoendelea nchini mwao na kuwafurusha kila uchao?

Sauti
3'32"