Ukiweza kutokomeza umasikini kwa wanawake, basi umeutokomeza kwa jamii: Paricia Makau
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya wanawake, moja ya changamoto kubwa inayowakabili wanawake kote duniani ni umasikini na ndio maana Umoja wa Mataifa uliuweka kutokomeza umasikini kama lengo namba 1 la maendeleo endelevu SDGs. Na unashirikisha na kualika wadau mbalimbali kushirikia katika vita hiyo na wengi wameitikia wito likiwemo shirika la kimataifa la kujitolea lisilo la kiserikali lijulikanalo kama Voluntary service Overseas (VSO).