UNCDF wamenipatia elimu na kuniunganisha na taasisi za kifedha – Mkurugenzi Nabuhima Foods
Aaron Mwimo kwa jina la utani Joti, ni mmoja wa watu wanaochangia utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs kwa kuleta ustawi bora kwa jamii yake wilayani Kibondo, mkoa wa Kigoma nchini Tanzania.
Bwana Mwimo alianzisha kiwanda kidogo cha kuchakata mazao ya wakulima kama vile mahindi na mihogo na akakipa kiwanda chake kidogo jina Nabuhima Food Supplies akisambaza unga katika mji eneo dogo la mji wa Kibondo hadi pale alipounganishwa na shirika la mitaji la Umoja wa Mataifa.