Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN/Ahimidiwe Olotu

Kijana Wajibika ya Restless Development yasongesha SDGs 16 nchini Tanzania

Lengo namba 16 la malengo  ya maendeleo endelevu, SDGs, yaliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2015 linalenga kuimarisha taasisi thabiti na zenye kusimamia haki kwa ajili ya kuwezesha uwepo wa jamii zenye amani na jumuishi. Mashirika ya kiraia katika nchi mbalimbali yamebeba jukumu la kusaidia na serikali kufanikisha lengo hilo na miongoni mwa mashirika hayo ni Restless Development ambalo nchini Tanzania kupitia mradi wa Kijana Wajibika linasaidia taasisi kujumuisha  watu wenye ulemavu na wasichana kwenye taasisi hizo.

Sauti
5'25"