14 FEBRUARI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo leo tunakwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuangazia changamoto za usalama mashariki mwa nchi hiyo hususan jimboni Ituri.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo leo tunakwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuangazia changamoto za usalama mashariki mwa nchi hiyo hususan jimboni Ituri.
Katika Siku ya Redio Duniani mwaka huu wa 2023, UNESCO inaangazia redio huru kama nguzo ya kujenga amani na kuzuia migogoro.
Hii leo ni siku ya redio duniani ambapo Umoja wa Mataifa unamulika nafasi ya chombo hicho kilichobuniwa takribani karne moja iliyopita katika kukuza na kujenga amani wakati huu ambapo pia ni miaka 75 tangu kuanzishwa kwa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa.
Nchini Burundi wakimbizi waliokimbia ghasia, wanaendelea kurejea nyumbani kutokana na hali ya amani kuzidi kuimarika, na hivi karibuni zaidi wakimbizi wamerejea kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC wakiwa na matumaini kutokana na kile wanachoshuhudia.
Hii leo jaridani tunaangazia siku radio duniani, na wakimbizi wanaorejea nyumbani Burundi. Makala tunakupeleka nchini DR Congo na mashinani tutamsikia Balozi Mwema wa UNHCR.
Nchini Tanzania tayari wanafunzi wa shule za msingi wameanza kunufaika na maadhimisho ya siku ya mikunde duniani kwa kutambua kuwa Umoja wa Mataifa unasisitiza matumizi ya mimea ya jamii ya mikunde katika sio tu kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwa kustahimili ukame, bila pia nafasi yake katika k
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kupeleka na kusambaza misaada nchini Uturuki au Türkiye na Syria ili kusaidia walioathiriwa na matetemeko makubwa ya ardhi yaliyotokea Jumatatu wiki hii na kujeruhi, kuua maelfu na kuharibu miundombinu.
Uwepo wa idadi kubwa ya wanawake na wasichana katika sekta ya sayansi ni faida kuwa kwa sekta ya sayansi na jamii kwa ujumla amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihimiza kuchagiza wanawake na wasicha kuingia zaidi katika sekta hiyo.
Hii leo jaridani tunaangazia wanawake na wasichana katika sayansi, na msaada wa binadamu mashariki ya kati kwa waathirika wa tetemeko la ardhi. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Misri, kulikoni?
Kama nilivyokudokeza hapo awali nabisha hodi nchini Burundi katika kambi ya wakimbizi ya Nyankanda iliyoko Mashariki mwa nchi hiyo kambi ambayo inahifadhi takriban wakimbizi 12,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. Kambini hapo wakimbizi wanapatiwa msaada unaotolewa kwa ushirikia