Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

13 FEBRUARI 2023

13 FEBRUARI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia siku radio duniani, na wakimbizi wanaorejea nyumbani Burundi. Makala tunakupeleka nchini DR Congo na mashinani tutamsikia Balozi Mwema wa UNHCR.        

  1. Katika siku ya redio duniani Umoja wa Mataifa unamulika nafasi ya chombo hicho kilichobuniwa takribani karne moja iliyopita katika kukuza na kujenga amani  wakati huu ambapo pia ni miaka 75 tangu kuanzishwa kwa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa.
  2. Nchini Burundi wakimbizi waliokimbia ghasia, wanaendelea kurejea nyumbani kutokana na hali ya amani kuzidi kuimarika, na hivi karibuni zaidi wakimbizi wamerejea kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC wakiwa na matumaini kutokana na kile wanachoshuhudia.
  3. Makala mwandishi wetu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Byobe Malenga anaangazia Redio Ngoma ya Amani, kituo cha redio cha mjini Fizi jimboni Kivu Kusini kinachohamasisha amani hususani katika maeneo ya mashariki mwa DRC.
  4. Na katika mashinani tutamsikia Balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR akipasa sauti kwa ajili ya wakimbizi na wote walio hatarini kutojumuishwa katika mijadala ya malengo ya maendeleo endelevu. 

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
10'40"