Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

14 FEBRUARI 2023

14 FEBRUARI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo leo tunakwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuangazia changamoto za usalama mashariki mwa nchi hiyo hususan jimboni Ituri. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo WHO, watoto katika maeneo ya migogoro na haki za raia nchini Zimbabwe. Mashinani tutasalia hapa makao maku ya Umoja wa Mataifa, kulikoni?

  1. Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO hii leo limeitisha mkutano wa dharura wa muungano wa chanjo ya virusi vya Marburg ili kujadili mlipuko mpya wa ugonjwa huo nchini Equatorial Guinea.
  2. Mfuko wa Umoja wa Mataifa unaohusika na kusongesha elimu kwenye maeneo yenye majanga na mizozo ya muda mrefu, Education Cannot Wait, au kwa lugha ya Kiswahili, Elimu Haiwezi Kusubiri umetangaza kutoa ruzuku ya dola milioni 7 nchini Syria kwa ajili ya kukuabiliana na dharura zilizopo lengo likiwa ni kusaidia wasichana na wavulana walioathiriwa na tetemeko ili waweze kuwa na mazingira salama ya kujifunzia na kupata usaidizi muhimu wa kisaikolojia, kijamii na ustawi unaohitajika.
  3. Na wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamemsihi Rais wa Zimbabwe kukataa kuufanya kuwa sheria, mswada ambao utaweka vikwazo vikali kwa asasi za kiraia na kuzuia haki na uhuru wa watu kujumuika nchini humo.
  4. Na katika mashinani tunamsikia Najat Maalla M'jid, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu Ukatili dhidi ya Watoto akihutubia Baraza la Ulama kuhusu watoto katika maeneo yenye migogoro.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
10'58"