Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sijasikia mlio wowote wa risasi, nyumbani Burundi hali ni shwarili - Aline

Sijasikia mlio wowote wa risasi, nyumbani Burundi hali ni shwarili - Aline

Pakua

Nchini Burundi wakimbizi waliokimbia ghasia, wanaendelea kurejea nyumbani kutokana na hali ya amani kuzidi kuimarika, na hivi karibuni zaidi wakimbizi wamerejea kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC wakiwa na matumaini kutokana na kile wanachoshuhudia.

Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR ikianza kwa kuonesha msafara wa magari uliobeba wakimbizi wa Burundi ukiingia kwenye lango kuu la mpaka wa taifa hilo, huko Bujumbura, ukitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. 

Baada ya kuingia mpakani, mmoja baada ya mwingine wakaanza kuteremka wakiwemo wanawake na watoto. Wamevalia barakoa zao, kujikinga na ugonjwa wa coronavirus">COVID-19. 

Kisha kwenye ukumbi wa eneo la mapokezi wakisubiri kusajiliwa na miongoni mwao ni Aline Niagara, mama huyu akiwa na watoto wake wanne, na anaelezea sababu ya kurejea nyumbani Burundi kutoka ukimbizi DRC, “Sasa ni mwaka mmoja na miezi miwili,  tangu nimeanza kusikia kutoka kwa wale waliorejea hapa nyumbani mapema. Wametuambia kuwa njooni, hakuna tatizo lolote nchini kwetu. Hakuna tatizo na majirani. Mkisaidiwa na UNHCR mje nyumbani, na ndio maana tumeamua kurejea na tayari tuko hapa.” 

Maafisa wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR wamejipanga hapa ambapo wanajaza nyaraka za waliorejea pamoja na kuchukua alama za vidole. Aline anazidi kufunguka juu ya kile anachokiona nchini mwake, “Moyo wangu uko na amani. Tulipovuka mpaka kupitia pale kwa maafisa wa forodha na kuingia hapa, nimeweza kuona watu wanatembea kwa uhuru. Tangu nimefika hapa, sijasikia mlio wowote wa risasi. Sijaona watu wakikimbia. Naona watu wako na amani.” 

Audio Credit
Edouige Emuresenge
Audio Duration
2'3"
Photo Credit
UNHCR Video