Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

10 FEBRUARI 2023

10 FEBRUARI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia wanawake na wasichana katika sayansi, na msaada wa binadamu mashariki ya kati kwa waathirika wa tetemeko la ardhi. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Misri, kulikoni?          

  1. Uwepo wa idadi kubwa ya wanawake na wasichana katika sekta ya sayansi ni faida kuwa kwa sekta ya sayansi na jamii kwa ujumla amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihimiza kuchagiza wanawake na wasicha kuingia zaidi katika sekta hiyo.
  2. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kupeleka na kusambaza misaada nchini Uturuki au Türkiye na Syria ili kusaidia walioathiriwa na matetemeko makubwa ya ardhi yaliyotokea Jumatatu wiki hii na kujeruhi, kuua maelfu na kuharibu miundombinu. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) lina lengo la kuwafikia watu nusu milioni katika nchi zote mbili ijapokuwa kuna changamoto za kiusalama katika baadhi ya maeneo.
  3. Makala tunakupeleka mkoa wa Njombe, kusini mwa Tanzania ambako huko leo kumefanyika maadhimisho ya siku ya mikunde duniani, ngazi ya kitaifa na John Kibambala wa redio washirika KIDS Time FM amezungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Itipingi katika halmashauri ya wilaya ya Njombe, ambao ni wanufaika wa mradi wa kilimo cha bustani na mlo shuleni unaopatia kipaumbele kilimo na mlo wa mazao aina ya mikunde, mradi unaofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO nchini humo.
  4. Na katika mashinani nampisha Dkt. Menatallah Elserafy kutoka Misri, ambaye ni Profesa msaidizi na mtafiti wa kuzingatia taratibu za ukarabati wa vinasaba au DNA katika Kituo cha Genomics cha Jiji la Sayansi na Teknolojia la Zuwail nchini humo. 

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Sauti
12'54"