OHCHR imetoa wito kwa wadau kuhakikisha uchaguzi mkuu wenye amani
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR, leo imetoa wito kwa wadau wote nchi Tanzania kuhakikisha uchaguzi mkuu unaofanyika kesho Jumatano Oktoba 28, unakuwa wa amani, jumuishi na shirikishi, kwa watu kuweza kupiga kura zao kwa uhuru bila hofu na vitisho.