Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

23 JULAI 2024

23 JULAI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika maoni ya vijana kuhusu SDGs, mmoja wao ni Monicah Malith Mkimbizi nchini Kenya kutoka Sudan Kusini akieleza alichotoka nacho kwenye mkutano wa HLPF. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani.

  1. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu imelaani ukimbizi wa mara kwa mara utokanao na amri za kuhama zinazotolewa na jeshi la Israeli dhidi ya raia huko kaskazini mwa Khan Younis, Ukanda wa Gaza.
  2. Barani Afrika, mashambulizi mapya yanayofanywa na vikundi vilivyojihami dhidi ya raia huko mashariki mwa Burkina Faso yamelazimu maelfu ya watu hao kukimbilia nchi jirani ya Niger ili kusaka usalama, wakati huu ambapo hali ya dharura inazidi kushamiri kwenye taifa hilo, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.
  3. Na hatimaye michezo ya olimpiki ya majira ya joto mwaka 2024 inaanza Ijumaa hii huko Paris, UFaransa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametuma ujumbe wake.
  4. Mashinani ikiwa jana Julai 22 Ripoti mpya kuhusu mapambano dhidi ya Ukimwi ilitolewa, hivyonampa fursa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS Winnie Byanyima akitahadhrisha kuhusu kuongeza kasi ya vita dhidi ya ukimwi.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

Audio Credit
Flora Nducha
Sauti
9'58"