Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

12 JULAI 2024

12 JULAI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia janga la kiafya na misaada ya kibinadamu nchini DRC, na mchakato wa uchaguzi mkuu nchini Sudan Kusini. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani inaturejesha nchini DRC, kulikoni?

  1. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC iko katikati ya janga la kiafya linaloongezeka limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani (WHO) na kusisitiza kwamba magonjwa ya milipuko yamezorotesha sana hali nchini humo katika miezi ya hivi karibuni kutokana na kuchochewa na ghasia na mafuriko.
  2. Wakati nchi ya Sudan Kusini ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu wake wa kwanza mwaka huu mwezi Desemba, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umeendesha kongamano la siku tatu la vyama vya siasa katika mji wa Rumbek ili kujadili masuala ambayo ni muhimu katika maandalizi ya uchaguzi huo.
  3. Katika makala Bosco Cosmas anatukutanisha na Katibu tawala katika kitivo cha Biashara na Uchumi kutoka chuo kikuu cha Mt. Agustino akieleza kuhusu jinsi kujua idadi ya watu kunavyoleta manufaa katika kuhakikisha maendeleo endelevu kwa jamii.
  4. Katika mashinani Deborah Dhra ambaye ni mama wa watoto wawili akitueleza jinsi shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Usaidizi wa Dharura, CERF linaboresha afya ya jamii zilizoathiriwa na migogoro kwa kuweka matanki na mabomba ya maji safi.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
10'1"