Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

uchaguzi mkuu

UNifeed Video

UNMISS wataka wanasiasa Sudan Kusini wapatie wanachi elimu ya kisiasa

Wakati nchi ya Sudan Kusini ikijiandaa kushiriki katika uchaguzi mkuu kwa mara ya kwanza kabisa tangu ipate uhuru, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS unaendesha makongamano na vyama vya siasa nchini humo. 

Ikiwa imesalia miezi 15 mpaka uchaguzi ufanyike hapo Desemba 2024 UNMISS wanasema lengo la kuandaa makongamano hayo nikujenga utamaduni wa kuwa na mazungumzo thabiti, kutatua changamoto zinazowakabili kuhusu utawala bora na kujenga kuaminiana miongoni mwa wanasiasa na jamii wanazozitumikia. 

Sauti
2'21"

02 AGOSTI 2023

Hii leo jaridani tunaangazia hali ya usalama nchini Sudan Kusini na mradi wa maji nchini Rwanda. Makala tunasalia huko huko Sudan Kusini na Mashinani tunakupeleka nchini Zimbabwe, kulikoni?  

Sauti
11'38"
UNMISS/Gregório Cunha

Nicholas Haysom: Hatua inahitajika sasa kwa ajili ya uchaguzi kwa wakati na wa huru na haki nchini Sudan Kusini

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), Nicholas Haysom ametahadharisha kwamba muda unazidi kuyoyoma kuelekea Sudan Kusini kufanya uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwezi Desemba mwaka ujao wa 2024 lakini bado masuala muhimu ya kuufanya uchaguzi huo uende kama ulivyopangwa bila kuchelewa hayajakamilika.

Sauti
2'18"